energy.gov.au

energy-theme-default

[Swahili/Kiswahili] Mwongozo wa mpangaji wa kutunza nishati na maji

A renter's guide to saving energy and water

Publisher

Department of the Environment and Energy

Date

auhitaji kuwa mmiliki wa nyumba ili kufaidika na vitendo vya nishati na kuhifadhi maji. Karibu theluthi moja ya Waaustralia wanaishi katika makazi ya kukodi, na hata kama kuna mapungufu juu ya nini unaweza kubadilisha katika nyumba yako ya kukodi, kuna njia za kupunguza bili yako na athari za mazingira, hata kama paneli za nishati na matangi ya maji ya mvua sio njia inayofaa. Kwa hakika, baadhi ya hatua za ufanisi zaidi unazoweza kuzichukua ili kuokoa nishati na maji zinalenga juu ya kufanya mabadiliko madogo ya tabia yako ya kila siku na hakuna gharama za fedha kwako hata kidogo.

Kama wewe umepanga kwa muda mfupi au muda mrefu, kuna njia nyingi rahisi, za gharama nafuu unazoweza kufanya ili kupunguza matumizi ya nishati na maji na kuokoa mamia ya dola katika kipindi cha mwaka bila kukatisha raha yako au kufurahia maisha.

Mawazo ya kutunza nishati

Ufanisi wa nishati (wakati mwingine huitwa ufanisi wa matumizi ya nishati) hasa ni kuhusu kutumia nishati kidogo kutoa utendaji ulio sawa na ule wa kawaida, mzuri na urahisi. Jaribu hatua hizi za vitendo ili kupunguza matumizi ya nishati katika kaya na bili za umeme.

  • Kuchagua vifaa vya nishati ya ufanisi. Vifaa vya Kaya vinatumia hadi asilimia 30 ya matumizi ya nyumbani kwako ya nishati, hivyo aina ya vifaa unavyochagua na jinsi unavyovitumia hufanya tofauti kubwa kwa matumizi ya nishati yako na bili. Kama unafanya manunuzi ya vifaa vipya, fikiria kununua aina mpya ya vifaa vya nishati. Angalia alama Energy Rating Label ili kujua ubora wa nishati—jinsi idadi nyota za nishati zinavyokuwa nyingi na ndivyo unavyoweza kutunza pesa.
  • Kudhibiti hali ya hewa yako. Kiasi cha asilimia 40 cha nishati ya nyumbani kinaenda kwenye kuweka joto na baridi. Katika majira ya baridi, fikiria kuweka themostati yako ya kuweka joto kwenye nyuzi 18–20. Katika majira ya joto, jaribu kuweka themostati yako ya baridi kwenye digrii 25–27. Kuweka kiasi cha nyuzi ya themostati hata moja juu (au chini) kinaweza kupunguza nishati inayotumika kuweka joto na baridi ya nyumba yako kwa asilimia 5 hadi 10. Wakati ukiweka kifaa cha joto au baridi kitumike, funga milango ya vyumba visivyotumika kwa kufunga milango ya vyumba vya ndani.
  • Kuziba mapengo na nyufa. Kwa kufanya nyumba yako imara na kuzuia kuvuja kwa joto au baridi kupitia kwenye matundu na kutoboka, unaweza kupunguza bili ya nishati kwa hadi asilimia 25. Jaribu mchanga wa kujazwa kwenye kitambaa rasimu (kama 'nyoka' ndefu) ili kuzuia hewa kukimbilia chini ya milango na tumia vizuizi vya hali ya hewa kwa ajili ya madirisha, bodi ya sakafu, bodi ya mbavuni, mataa ya angani na vingine. Zungumza na mwenye nyumba yako kabla ya kufaa vizuizi vyovyote vya hewa.
  • Kuboresha ufanisi wa madirisha. Kuzuia kupoteza joto hasara kwa kuweka mapazia yanayofaa na kupofua kwa mtego wa safu ya hewa karibu na dirisha. Unaweza pia kufungua mapazia katika majira ya baridi ili jua liingie ndani wakati wa mchana na kuyafunga kabla ya giza kuingia. Vile vile, ni vizuri kufunga mapazia wakati wa muda wa joto katika siku ya wakati wa majira ya joto.
  • Kuchagua feni kuliko kiyoyozi. Feni ya kwenye dari na tako ukutani inagharamu karibu asilimia moja kwa saa inapokuwa inafanya kazi na inazalisha gesi ndogo chafu kuliko ile ya viyoyozi. Feni zinasaidia kusambaa hewa na zinaweza kutumika kuboresha ufanisi wa mifumo ya baridi ya hewa ikiwa ni pamoja na kusambaa hewa ya moto na kuboresha ufanisi katika majira ya baridi.
  • Kuhamia kwenye mataa yenye ufanisi ya nishati. Karibu asilimia 12 za matumizi ya nishati majumbani huenda kwenye mataa. Kwa kutumia mataa ya ufanisi ya nishati na kutumia mataa ya ufanisi unaweza kupunguza nusu ya gharama ya kwenye mataa. Kubadilisha globu za mataa ya aina ya zamani yenye nguvu kubwa (CFLs) au diodesi za mwanga kutotoa moshi (LEDs) ni njia ya ufanisi ya kuokoa gharama za nishati. CFLs inatumia karibu asilimia 20 ya nishati ya mataa ya mwanga na inaweza kudumu kati ya mara 4 hadi 10 zaidi.
  • Nguvu ya umeme inayosubiri Vifaa vingi na njia za umeme, kama vile chaja ya simu, viweko vya mchezo, sehemu zote za oveni za wimbi mikro na redio zinaendelea kuteka nguvu ya umeme wakati hazitumiki. Nguvu hii ya kusubiri inaweza kuchukua asilimia 10 ya matumizi ya kaya yako ya umeme. Kwa kuzima vifaa na soketi za umeme kwenye ukuta wakati ukimaliza kuvitumia unaweza kupunguza matumizi ya nishati na bili zako. Kama ukiwa na umeme wa mwanga kidogo usizimwa au saa bado unatumia nguvu.
  • Friji na jokofu. Joto la juu la friji yako ni kati ya nyuzi 3 na 5; au kati ya nyuzi 15 na nyuzi 18 Celsius kwa ajili ya jokofu lako. Kila nyuzi iliyo ya chini inahitaji asilimia 5 zaidi ya nishati. Kuboresha ufanisi wa friji yako na jokofu kwa kuondoa barafu za baridi zilizojengana na kuacha pengo la sentimita 5–8 karibu nayo kwa uingizaji hewa. Kama una friji ya pili kwa ajili ya burudani, iwashe tu wakati unaihitaji.
  • Kuosha na kukausha nguo. Wakati mashine inaosha, okoa nishati na maji kwa kutumia maji ya baridi, na mzunguko mfupi iwezekanavyo, rekebisha kiasi cha maji yako yalingane na ukubwa wa mzigo wa nguo na subiri mpaka una nguo za kutosha kwa ajili ya mzigo kamili. Kausha nguo kwenye kamba ya nguo badala ya mashine ya kukausha ya umeme -haina gharama.

Njia za kuokoa maji

Kuwa mtumiaji wa maji wa ufanisi husaidia kujali kila tone ya maji na dola. Kuna vitendo vingi vya kuchukua katika kutumia maji kwa busara nyumbani na katika bustani ili kutunza maji vizuri kwa ajili ya siku zijazo.

  • Zingatia vifaa vya maji vya ufanisi na samani. Wakati unanunua samani mpya , zingatia vifaa vya ufanisi vya maji. Angalia Water Efficiency Labelling and Standards (WELS).
  • Kutumia mabomba kwa ufanisi. Bomba linalovuja kwa kiwango cha mara moja kwa njia ya matone kwa sekunde inapoteza zaidi ya lita 12,000 za maji kwa mwaka. Okoa maji kwa kutengeneza mabomba yoyote yanayovuja haraka iwezekanavyo. Unaweza kupunguza matumizi ya maji yako kwa kufunga viingiza hewa Viingiza hewa vinapunguza mtiririko wa maji na inaweza kufungwa kwa ndani au nje ya mabomba. Unaweza kutakiwa kuzungumza na mwenye nyumba yako kabla ya kufanya mabadiliko.
  • Kufunga vichwa vya mabomba ya kuogea vya ufanisi wa maji. Kama una vichwa vya mabomba ya kuogea vilivyozeeka, jaribu kuuliza mwenye nyumba yako ili aweze kuvibadilisha kuweka vyenye vinatumia maji kwa ufanisi na unaweza kuokoa zaidi ya dola 160 kwa mwaka katika bili ya nishati na maji.
  • Kusafisha vyoo. Wakati wa kutumia visukumo viwili vya choo, chagua kutumia nusu ya kisukumo pale inapostahili. Kama mwenye nyumba yuko anarudishia choo chenye kisukumo kimoja, fikiria kumshauri aweke chenye visukumo viwili vyenye ufanisi wa kutunza maji maana vinaweza kuokoa mpaka lita 55 kwa mtu mmoja kila siku. Kama hii sio chaguo, unaweza kununua kifaa cha kutunzia maji au kutumia chupa ya plastiki iliyojaa maji katika kisima kupunguza ujazo wa maji.
  • Kupunguza matumizi ya maji ya bustani. Umwagiliaji wa jadi inaweza kutumia hadi asilimia 90 ya maji ya bustani yako. Unaweza kupunguza hii kwa kuweka kifaa ili kupunguza sentimita 4 au zaidi. Unaweza pia kupunguza matumizi yako ya bustani kwa kuboresha mazoea ya umwagiliaji na kuchagua vifaa vyenye ufanisi kwa maji.

Rasilimali za wapangaji

Zungumza na mwenye nyumba wako au wakala wa majumba

Matengenezo, huduma au matengenezo, ikiwa ni pamoja na maboresho yoyote endelevu, kwa kawaida yanahitaji ruhusa (na fedha) kutoka kwa mwenye nyumba wako. Kila jimbo na wilaya lina sheria mbalimbali za wapangaji, hivyo ni muhimu kufanya utafiti wako na kuomba ruhusa kabla ya kufanya mabadiliko yoyote ya nyumba.
Baadhi ya mambo ya kuzingatia wakati unapozungumza na mwenye nyumba wako au wakala wa majumba kuomba maboresho endelevu ni pamoja na:

  • Msamaha na msaada. Kuna aina mbalimbali ya msamaha wa serikali na misaada inayopatikana kwa wamiliki wa nyumba kwa ajili ya kufanya maboresho endelevu. Kukusidia namahitaji yako ni vizuri kufanya utafiti kwa niaba ya mpangishaji wako na tafuta kujua msamaha na msaada ambao unaendana na mazingira yako.
  • Punguzo la kodi Maboresho mengi ya majengo yaweze kutumia nishati ndogo, ikiwa ni pamoja matengenezo na marekebisho, yana punguzo la kodi. Unaweza kutakiwa kuangalia kwenye mwongozo wa Ofisi ya Kodi ya Australia wa wamiliki wa majengo ya kupangisha ili kujua ni ipi inahusika kwa kaya yako na fikisha habari njema kwa mpangishaji wako.
  • Faida za uwekezaji Kwa kuwekeza katika maboresho ya majengo ambayo inaleta nishati ya nyumba na ufanisi wa maji, mpangishaji wako anaweza kuongeza thamani ya mali, na kuifanya kuvutia zaidi kwa wanunuzi na wapangaji wa baadaye.

Hakikisha unaweka maombi kwa mpangishaji wako au wakala wa majengo kwa maandishi. Ni vizuri kutunza kumbukumbu ya maombi yote pamoja na mikataba kutoka kwa mpangishaji wako au mawakala wa majumba ya kufanya mabadiliko au maboresho.

Je unahitaji kujua na kuokoa zaidi?

Aina nyingi za mazoezi juu ya nishati, uchafu, maji na kusafiri kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na habari kuhusu msaada wa serikali zipo kwenye lugha ya Kiswahili kwenye www.energy.gov.au website.

Kanusho

Jumuiya ya Madola haina dhamana ya uhalisi wa waraka ambayo tafsiri ilifanywa na haitoi maoni yoyote ya usahihi wake au vinginevyo kuhusu habari zozote zilizomo katika hati ya awali au tafsiri hii. Jumuiya ya Madola haitoi uhakika wowote kuhusiana na tafsiri hii, ikiwa ni pamoja na usahihi wa tafsiri. Jumuiya ya Madola na maafisa wake, wafanyakazi au mawakala hawahusiki kwa uharibifu wowote, hasara katika kuumia iwe ya moja kwa moja au isiyohusiana kutokana na matumizi yoyote ya mtu au yaliyotegemea tafsiri hii, iwe au isiwe imetokana na kujitegemea habari au ushauri uliotolewa na mashirika mengine.

This translation was funded as part of the Australian Government Multicultural Access and Equity policy.