energy.gov.au

energy-theme-default

[Swahili/Kiswahili] Mawazo tano enye busara kwa kuokoa nguvu ya umeme na pesa nyumbani kwako

5 bright ideas for saving energy and money in your home

Publisher

Department of the Environment and Energy

Date

Wakati ambapo bei ya nguvu ya moto inainuka, wengi wetu wanaangalia njia za kutumia idadi kidogo ya nguvu ya moto nyumbani. Habari njema ni kuwa kuna vitu nyingi rahisi, bila gharama ambazo unaweza kufanya hivi sasa. Kwa kujaribu mawazo haya mengine na kufanya mabadilisho chache katika mazoea za kila siku, unaweza kuokoa pesa na kusaidia mazingira bila kupoteza starehe.

 1. Pungunza utumiaji wa maji moto

  Maji moto inatumia kiasi ya asilimia ishirini na tano ya gharama ya kawaida ya moto nyumbani. Njia ya kuipunguza ni kwa kusafisha nguo kwa maji baridi na kuongoja hadi wakati una nguo kiasi inayojaza, tumia mashine ya kuosha viombo tu wakati vyombo vimejaa, weka sehemu ya kichwa ya kutoa maji ya kuoga kuwa na mfuriko kidogo. (Hii italipa kivyake kwa wakati mfupi) na kuoga kwa muda mfupi.

 2. Kuchagua chombo yenye kufaa

  Vyombo vya nyumbani vinaweza kugharamia nusu tatu ya gharama ya moto yako. Kama unanunua friji mpya, friza, televisheni, mashine ya kuosha nguo, mashine ya kukausha nguo, mashine ya kuosha vyombo au mashine ya kupasha hewa baridi, angalia maelezo ya kukadiri kiasi ya nguvu inayotumia—ikiwa ina nyota nyingi, chombo hii itatumia nguvu kidogo ya moto. Chombo yenye nyota ya juu inaweza kugharimu bei ya juu, lakini kuchagua chombo bei rahisi yenye nyota ya chini inaweza kugharimu zaidi kwa wakati zijazo.

 3. Kutumia chombo kwa busara

  'Nguvu ya moto kwa kusimamisha moto' inayotumiwa na chombo kama vile machine ya kupasha chakula moto, televisheni na chombo ya kucheza michezo inaweza kugharimia asilimia kumi ya bei ya nguvu ya moto yako. Kama inaonyesha taa kidogo au saa—inatumia moto. Gharama ya matumizi yake inaweza kupunguzwa kwa kuzima chombo kutoka kwa ukuta wakati hazitumiwi. Kuondoa vyombo zaidi ya friji, friza ambazo hazihitajiwi, na kukausha nguo kwenye jua badala ya mashine ya kukausha.

 4. Kupasha joto na kupasha baridi kwa njia inayofaa

  Kwa kila kadiri ya kupasha joto au baridi inayo ongezwa, matumizi ya nguvu ya moto itaongeza kwa angalau asilimia tano hadi kumi. Ili kutawala vizuri gharama yako, fikiria kuhusu kuweka kidude cha kupima kiasi ya joto kwa kiasi ya kadiri selisiasi kumi na nane hadi ishirini wakati wa majira ya baridi na hadi kadiri selisasi ishirini na tano hadi ushirini na saba wakati wa majira ya joto. Unaweza kuweka joto unayotumia kwa kufunga milango ya ndani na kupasha joto au baridi kwa chumba ambazo unatumia.

 5. Kukinga nyumba yako kutumia kizuizi

  Kutumia kizuizi ni njia rahisi na gharama ya chini kwa kuweka nyumba yako starehe na kuokoa hadi robo ya gharama yako ya kupasha joto na baridi. Kuziba mwanya kwenye milango, sakafu, madirisha, na kutumia mchanga iliyojazwa au nguo 'soseji' kizibo ni jia mengine ya 'kufanya mwenyewe'.

Ungependa kujua na kuokoa zaidi?

Idadi kubwa ya vidokezo ya kufaa kuhusu moto,utumiaji ya upotevu, maji na usafiri inayofaa na pia maelezo kuhusu usaidizi kutoka serekali iko kwa lugha ya kiingereza kwenye mtandao energy.gov.au.